Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas ametoa wito wa kutafuta suluhisho kunakohusisha pande tofauti tofauti na kumshutumu Rais wa Marekani Donald Trump kwa kujichukulia maamuzi bila ya kushirikisha wengine.
Akizungumza jana jioni katika mkutano huo wa Munich, Maas aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kuongezeka kwa nguvu za China kunahitaji nchi za Ulaya na Marekani kufanya kazi kwa pamoja, akigusia pia hatua ya Trump ya kuongeza bei ya bidhaa za chuma kama jambo linalotishia nafasi za ajira Ulaya.
Maamuzi ya Marekani yatajwa hayana tija
Waziri huyo ya mambo ya kigeni wa Ujerumani pia ameishutumu Marekani kwa kujiondoa kutoka mkataba wa kinyuklia uliofikiwa kati ya Iran na nchi zenye nguvu zaidi duniani akisema Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zinajaribu kuyadumisha makubaliano hayo kwani yakisambaratika, basi kanda ya Mashariki ya Kati huenda ikatumbukia katika mizozo zaidi.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema umoja huo unalenga kuyadumisha makubaliano hayo yanayoidhibiti Iran kutoendelea na mpango wake wa kuunda silaha za kinyuklia akiongeza ni muhimu kwa usalama wa Ulaya.
Awali, makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alikuwa ameishutumu Iran kwa kile alichokitaja inapanga mauaji mapya ya Halaiki ya Wayahudi kwa kuendelea kuwa hasimu wa Israel na kuingilia mizozo ya Syria, Lebanon, Iraq na Yemen.
Ikumbukwe kuwa Iran imejitolea kuwatetea wapalestina ambao wamedhulumiwa ardhi zao na Israel pia imekuwa ikiisaidia Lebanon katika kupambana na majeshi vamizi ya Israel. Na kuwa upande wa Syria na Iraq, Iran ilipeleka majeshi yake ili kupambana na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani na washirika wake, huko Yemen, Marekani, Saudia arabia na matataifa mengine zaidi ya 11 yamekusanyika na kuwasambulia wananchi wanaoungwa mkono na Iran kwa lengo la kumrudisha madarakani rais ambaye wananchi hawamtaki. Baada ya Marekani kushindwa katika sehemu hizo imeamua kuiwekea vikwazo vikali Iran ili kuidhoofisha.
Mwisho wa habari / 291